Mpaka sasa hakuna ishara yeyote ya uhakika ya kufikia makubaliano katika mazungumzo ya mjini Lausanne Uswisi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema mjini Brussels "hakuna makubaliano "kwa kila hali"yatakayofikiwa.Makubaliano yanabidi yahakikishe kwamba Iran haitokuwa na uwezo wa kutengeneza silaha za nyuklia.Steinmeier na waziri mwenzake wa mambo ya nchi za nje kutoka Ufaransa na Uengereza,Laurent Fabius na Philipp Hamond wamezungumza na waziri mwenzao wa Iran Mohammed Jawad Zarif kuhusu uwezekano wa kuondolewa vikwazo vya nchi za magharibi.Kabla ya hapo waziri Zarif alikutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry mjini Lausanne nchini Uswisi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema ikiwa mazungumzo yatashindwa,Marekani itazidi kuishinikiza Iran.
Kwa upande wa Iran inasema kuwa, haina nia yakutengeneza silaha za nyuklia, na kama itaamua kutengeneza basi hakuna wakuizuia, na kuongeza kuwa haitishwi na vikwazo kwani imekuwa kwenye vikwazo kwa zaidi ya miaka 36, na vikwazo havikuweza kuiathiri Iran kwa kiasi kikubwa bali vikwazo hivyo vimekuwa ni sababu ya Iran kusonga mbele kielimu na nyanja nyingine.
Viongozi wa Iran wanasema kuwa wanania yakufikia makubaliano lakini inatakiwa makubaliano hayo yawe na misingi ya kimantiki nasi makubaliano ya mashinikizo.
Marekani na washirika wake wanajaribu kuingiza masuala ambayo yako nje ya mada ya nyuklia katika mazungumzo ya nyuklia, jambo ambalo kinapingwa vikali na serikali ya Iran.
Marekani na Israel wanadai kuwa Iran inatakiwa iache kudhamini magaidi wa Hamas na Hizbullah, na upande wa pili unasema kuwa Marekani, Israel na washirika wao, waache kudhamini magaidi wa Daesh na Al Nasr ambao wanaua watu na kufanya jinai zao nchini Syria na Iraq.
Kufikiwa kwa makubaliano hayo ya nyuklia kutahesabika ni jambo la pekee kutokea katika historia ya siasa baina ya pende mbili za Marekani na Iran.